A+ PC DOCTOR

A+ PC DOCTOR

Sunday, 3 September 2017

Alichokisema chid Benz kuhusu collabo yake na 2pac

Rapper maarufu Bongo, Chid Benz ameibuka na kusema kuwa amefanya collabo na rapper mkongwe wa Marekani, marehemu Tupac Shakur huku akiapa kumleta Bongo. Chid Benz ambaye pia alikanusha kukamatwa na kutumia Dawa za Kulevya alidai kuwa amekuwa akiongea na rapper huyo wa Marekani na tayari wamerekodi hadi vipande vya video kwa ajili ya comeback yake.

 “Tupac yupo hai, yupo Cuba, nilienda Cuba juzi juzi alinipigia simu nionane nae, anataka kurudi kwenye game na kuonesha yupo hai kwahiyo alinipiga akaniuliza mwanangu Chid tunafanyaje, nikamwambia tusifanye ngoma kwanza tufanye ki’movie kwanza” Chid Benz alifunguka kwenye ENewz ya EATV.